• Latest News

  Monday, April 21, 2014

  JE ! KUWA NA MRADI NI LAZIMA UWE NA FEDHA NYINGI?

  KILIMO CHA BUSTANI NA MAUA CHA DADA YASINTA...KARIBUNI !!!!!

  Habari zenu..kuna wengi wameniuuliza vipi kuhusu bustani pia mapishi nipi na bustani ipi ila pilikapilika ni nyingi na hizi likizo lakini leo nimeona sio mbaya nichukue muda na kuwaonyesha maendeleo ya bustani yangu...Karibuni
   
   
   Nyanya zimeanza kukomaa karibu nitakula
   Kushoto ni mchicha na kulia ni figiri  mnaona ilivyokua
   Njegere zimeanza kuchanua
   Viazi mviringo(matosani)  navyo vimwanza kuchanua
   Mdada huyu ni mpenzi wa maua pia mawe hapa mnaona maua yako yanavyoendelea.
  Kwa kuwa mtundu nikajaribu kupandikiza pilipili pia maana pitiku bila pilipili mmmmhh na matokeo ni haya
  Sikuchoka nikajaribu kupandikiza dodoki  Nanasi na tangawizi---Dodoki kwenye hicho chombo cha bluu, nanasi chombo cha blauni na tangawizi chombo cheupe. Kwa msingi kwa kweli unaweza kupanda kila kitu na kuvuna. Haya nawatakieni Alhamisi njema na karibuni kula mazao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  2 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: JE ! KUWA NA MRADI NI LAZIMA UWE NA FEDHA NYINGI? Rating: 5 Reviewed By: Kilimo mifugo
  Scroll to Top