• Latest News

  Thursday, April 10, 2014

  NDIKANA KALI - EAST COAST FEVER


  Ugonjwa huu hushambulia wanyama kama ng'ombe, mbuzi na kondoo na husababishwa na vimelea vijulikanavyo kama Theileria parva ambavyo vusambazwa na kupe wekundu wa kwenye masikio wajulikanavyo kama Rhepicephalus Appendiculatus, ugonjwa huu usipodhibitiwa unaweza kusababisha vifo vya wanyama wengi sana na pia ni aghali kuutibu kulinganisha na magonjwa mengine


  KUPE WEKUNDU KWENYE MASIKIO YA NG'OMBE

  DALILI ZA UGONJWA HUU
  Homa kali, mnyama kushindwa kupumua vizuri,  kukohoa pamoja na kutoa makamasi, kuharisha na kuvimba matezi

  MATIBABU
  Mnyama inabidi apigwe sindano ya dawa za  PARVAQUONE au BUTALEX kiasi cha ml 20 (soma kimbatanisho cha dawa kwa maelezo zaidi) na kurudia baada  ya siku moja kupita, yaani ukuchoma leo unarudia dozi kesho kutwa, pia mnyama achomwe dawa ya OTC20% kipindi chote cha matibabu  KINGA
  Kinga kubwa ya ugonjwa huu ni kuhakikisha kwamba mifugo yako inaoga mara kwa mara kwenye majosho au kwa kuwanyunyuzia dawa za kuua wadudu wa mifugo

  NG'OMBE WAKIOGESHWA KWENYE DAWA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: NDIKANA KALI - EAST COAST FEVER Rating: 5 Reviewed By: Kilimo mifugo
  Scroll to Top