• Latest News

  Saturday, April 26, 2014

  TANGAZO LA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA STASHAHADA NA ASTASHAHADA KATIKA WAKALA WA VYUO VYA MAFUNZO YA MIFUGO (LIVESTOCK TRAINING AGENCY) KATIKA MWAKA WA MASOMO 2014/15  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI
  WAKALA WA VYUO VYA MAFUNZO YA MIFUGO - LITA  Telegram: “Mifugo”
  Simu:  255 022 2861910
  Fax: 255 022 2861908
  E-mail: litahq@yahoo.com

                                       
  In reply please quart:   


  Temeke Veterinari,
  Barabara ya Mandela,
  S. L. P.  9152,
  DAR ES SALAAM

   
   

                                                 


  TANGAZO LA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA STASHAHADA NA ASTASHAHADA KATIKA WAKALA WA VYUO VYA MAFUNZO YA MIFUGO (LIVESTOCK TRAINING AGENCY) KATIKA MWAKA WA MASOMO 2014/15

  1.    Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) inatangaza nafasi za
  mafunzo katika ngazi ya Astashahada na Stashahada kama ifuatavyo:

  ·         Stashahada ya Afya na Uzalishaji wa Mifugo (Diploma in Animal Health and Production - DAHP)
  ·         Astashahada ya Afya na Uzalishaji Mifugo (Animal Health and Production Certificate - CAHP)
  ·         Astashahada ya Ufundi Sanifu wa Maabara (Certificate in Veterinary Laboratory Technology - CVLT)

  2.    Katika mwaka wa fedha wa 2014/2015, Serikali kupitia Wakala wa Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo (LITA) itatoa mafunzo kwenye Kampasi zake sita na vituo vyake viwili Tengeru, Mpwapwa, Morogoro, Buhuri, Madaba, Temeke, Vituo vya Mabuki na Kikulula. Kampasi ya Temeke haina malazi hivyo watakaojiunga itabidi wajitegemee kwa malazi. Pia katika Kampasi zetu kutakuwa na nafasi chache kwa wanafunzi watakaopenda kukaa nje ya Chuo (Private day students).

  3.    Wakala inakaribisha maombi kutoka kwa vijana waliomaliza kidato cha Nne wanaotaka kujiunga na mafunzo ngazi ya Astashahada. Pia vijana waliomaliza Kidato cha Sita na wale wenye Astashahada katika fani zinazohusiana na kozi wanazoomba kwa ajili ya kujiunga na mafunzo ngazi ya Stashahada.


  4.    Kampasi zitakazohusika na mafunzo hayo ni kama inavyooneshwa kwenye jedwali hapa chini:

  Na
  KAMPASI / KITUO
  ANUANI
  KOZI ZITOLEWAZO
  1.     
  TENGERU
  S.L.P 3101 Arusha
  DAHP & CAHP(Bweni na kutwa)
  2.     
  MPWAPWA
  S.L.P 51 Mpwapwa
  DAHP & CAHP(Bweni na kutwa)
  3.     
  MOROGORO
  S.L.P 603 Morogoro
  DAHP& CAHP (Bweni na kutwa)
  4.     
  BUHURI
  S.L.P 1483 Tanga
  CAHP(Bweni na kutwa)
  5.     
  MADABA
  S.L.P 568 Songea
  DAHP & CAHP(Bweni na kutwa)
  6.     
  TEMEKE
  S.L.P 9254 DSM
  CVLT (Kutwa)
  7.     
  MABUKI
  S.L.P 352  Mwanza
  CAHP (Bweni na kutwa)
  8.     
  KIKULULA
  S.L.P 147  Karagwe
  CAHP (Bweni)

  5.     Sifa za mwombaji

  i) Stashahada (Diploma)
  ·           Awe amefamemaliza elimu ya Kidato cha Sita kufaulu masomo matatu ya Sayansi kati ya Baiolojia, Kemia, Fizikia, Hisabati, Jiografia na Kilimo. Kiwango cha chini cha ufaulu kitakachomwezesha muombaji kukubaliwa ni cha subsidiaries mbili kwenye masomo ya sayansi.
  AU
  ·           Awe amemaliza mafunzo ya Astashahada (Certificate) katika fani ya Animal Health and Production (AHPC), Agrovet au Certificate in Agriculture and Livestock Production (CALP) ambayo ni sawa na NTA Level 5 kwenye vyuo vilivyosajiliwa na NACTE

  ii) Astashahada (Certificate)
  ·           Awe amemaliza Kidato cha Nne na kufaulu masomo matatu ya sayansi kati ya Baiolojia, Kemia, Fizikia, Hisabati, jiografia na Kilimo. Kiwango cha chini cha ufaulu kitakachomwezesha muombaji kukubaliwa ni cha alama ya D kwenye masomo ya sayansi.


  6.    Masharti ya Uombaji

  ·           Mwombaji atume fomu za maombi ya kozi anayotaka kusomea  kwa kujaza fomu akiambatanisha nakala (photocopies) za vyeti vyake vya elimu, pamoja na cheti cha kuzaliwa.
  ·           Fomu inapatikana kwenye Kampasi zetu, vituo vyetu vyote na Tuvuti ya Wizara Website: www.mifugouvuvi.go.tz

  ·           Fomu irudishwe na Bank pay-in slip ya Tshs 20,000/= iliyolipwa LITA Revenue Account, NMB Morogoro, Acc. No. 22110003142

  ·           Fomu zote zitumwe Makao Makuu ya Wakala na siyo kwenye Kampasi za Mafunzo kwa kutumia anuani au barua pepe ya hapo chini.

  ·           Waombaji watakaoomba nafasi za kutwa itabidi wajiandae kutafuta sehemu za malazi na kuonyesha Kampasi atakayopenda kusomea.

  7.    Gharama za Mafunzo

  Gharama za mafunzo zimeonyeshwa  kwenye fomu ya maombi ambayo inapatikana kwenye Kampasi, vituo vya Wakala na tovuti ya Wizara Website: www.mifugouvuvi.go.tz

  8.    Mwisho wa kupokea maombi

  Mwisho wa kupokea fomu za kujiunga na masomo ni tarehe 30/06/2014.

  9.    Taarifa kwa watakaochaguliwa

  Majina ya watakaochaguliwa yatatangazwa kwenye magazeti ya Daily News na Habari Leo, kwenye mbao za matangazo za Wizara, Kampasi, vtuo vyake vyote na kwenye tovuti: www.mifugouvuvi.go.tz
  LITA) KA
  10. Utaratibu wa kutuma fomu za maombi

  Fomu za maombi zitumwe kwa:  MTENDAJI MKUU,
  WAKALA WA VYUO VYA MAFUNZO YA MIFUGO - LITA,
  S.L.P. 9152,
  DAR ES SALAAM


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TANGAZO LA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA STASHAHADA NA ASTASHAHADA KATIKA WAKALA WA VYUO VYA MAFUNZO YA MIFUGO (LIVESTOCK TRAINING AGENCY) KATIKA MWAKA WA MASOMO 2014/15 Rating: 5 Reviewed By: Kilimo mifugo
  Scroll to Top