Wadau, naamini kuwa hamjambo na mmeamka salama. Nami pia Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniamsha salama. Wale wagonjwa tuwaombee kwa Mwenyezi Mungu awajaalie wapone haraka. Wale waliofikwa na mauti, tumuombe Mwenyezi Mungu awape mwisho mwema.

Wadau, uwasilishaji wa Taarifa za Kamati 12 za Bunge Maalum umeanza juzi Alhamis tarehe 10 April 2014. Katika siku hiyo, jumla ya kamati 4 ziliwasilisha taarifa zake ambazo ni kamati namba 2,5,9 na 11. Aidha, Jana Ijumaa kamati nne ziliwasilisha taarifa zake ambazo ni kamati namba 1,8,10 na 12. Hivyo, hadi leo Kamati nne hazijawasilisha taarifa zake ambazo ni kamati namba 3,4,6 na 7. Kwa vile Bunge kwa siku ya leo linaishia saa saba mchana, ni wazi kuwa kamati mbili tu zitawasilishwa. Kamati mbili zitakazobaki zitawasilisha siku ya Jumatatu ijayo.

Mpaka sasa, kuna mfanano usio wa kawaida kwa taarifa zote. Taarifa za walio wengi kwa kamati zote zinafanana ikiwa ni pamoja na ibara zinazofanyiwa marekebisho, aina ya marekebisho na sababu za marekebisho. Mathalan, katika Ibara ya Kwanza, walio wengi wanapendekeza marekebisho badala ya neno shirikisho, wanapendekeza litumike neno Jamhuri. Pia badala ya neno Tanganyika, wanataka itumike Tanzania Bara. Halikadhalika katika Ibara ya 60 juu ya muundo wa muungano, walio wengi kwa kamati zote wanapendekeza muundo wa serikali mbili badala ya serikali tatu zilizopo kwenye rasimu ya katiba. Sababu kuu inayotolewa ni Hati ya Muungano

kwa upande wa maoni ya walio wachache, wao ni copy and paste kama ilivyo kwa walio wengi. Wao wanataka mapendekezo yaliyopo kwenye Rasimu ya Katiba yaendelee. Sababu kubwa wanayotoa ni kwamba Maoni ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ni Maoni ya Wananchi. Pia maoni ya walio wachache wanatumia rejea zile zile kuimarisha hoja zao. Mathalan, wamekuwa wakitumia na kutetea takwimu zile zile za Warioba, wamekuwa wakirejea tume zile zile za akina Kisanga na Nyalali.

Na wamekuwa wakinukuu kazi zile zile za wasomi mbalimbali kama akina Prof Shivji, Paramagamba Kabudi nk. Hali hii imefanya baadhi ya wadau kuhoji uwepo wa utitiri wa kamati ilhali maoni yao yanafanana. Wanasema kuwa mfumo uliotumika wakati wa kujadili Rasimu ya Katiba ungetumika ambapo watu waliotoka makundi mbalimbali waliounda kamati moja chini ya Prof Costa Mahalu na walitoa mapendekezo ya rasimu ya kanuni inayokubalika. Wanasema kuwa hali hiyo ingeokoa muda zaidi na wabunge wangepata muda zaidi wa kujadili. Hayo ni maoni tu ya wadau.

Karibu kwamjadala

----------------------------

- Mwenyekiti ameingia na dua imesomwa. Kamati inayoanza kuwasilisha taarifa yake ni kamati namba tatu ambayo inasomwa na mwenyekiti wake Dr Fransis Michael

- MAONINYA WALIO WENGI
* Ibara ya kwanza wanapendekeza iwe Jamhuri badala ya shirikisho. Sababu wanayotoa ni Sheria ya mabadiliko ya katiba, Ibara ya kwanza inataka uwepo wa Jamhuri ya Muungano. Wanasema kuwa hata Kamati ya Warioba ililitambua hili na ndani ya randama ya tume, ukrasa wa 3 imetaja uwepo wa Jamhuri. Pia wanasema kuwa makubaliano na sheria ya mwaka 1964 yanatambua uwepo wa Jamhuri na hivyo wanapendekeza makubaliano hayo yawe nyongeza ya Rasimu ya Katiba. Walio wengi wanashangaa wachache kutamka hati ya Muungano ilhali Tume ya Jaji Warioba inaitambua.

- Dr Fransis anasema kuwa Hati ya Muungano ni sahihi na Wazanzibari walihusika kuiridhia. Amenukuu maneno ya Marehemu Thabit Kombo wakati akichangia hoja ya kuridhia hati hiyo kwenye Bunge la Tanganyika.

- Dr Fransis anasema kuwa kuna watu hawana utashi wa muungano huu kudmu na hivyo wanataka uwepo wa serikali tatu ili wavunje muungano

- Mwenyekiti anatoa ufafanuzi kuwa wanaowasilisha wanaruhusiwa kutoa ufafanuzi wa hoja ili mradi hawako nje ya mada na wahakikishe kuwa wanaacha dakika zisizopungua 15 kwa ajili ya kusoma maoni ya wachache

- Dr Fransis anamnukuu Juma Duni Haji wakati aki wind up election campaign kwa chama cha CUF huko Zanzibar mwaka 2005 aliposema kuwa "Wakati wa kutawala watu weusi Zanzibar umeisha"

- Anasema kuwa muungano wa shirikisho unaweza kusababisha matatizo mengi ambayo yatahatarisha muungano wetu. Pia kukiwa na shirikisho, kila nchi itakuwa na mila na desturi zake ambazo zinaweza kusababisha mgongano na hivyo kuweza kuhatarisha umoja na mshikamano wetu

- Dr Fransis anasema kuwa muungano wetu ni wa udugu hasa kwa vile wameoleana katika pande zote

- Dr Fransis anapendekeza kuwa mipaka ya nchi isitenganishwe baina ya Zanzibar na bara

- Dr Fransis anapendekeza ziwepo Ibara ambazo zitahakikisha hifadhi na matumizi sawa ya ardhi na vitu vilivyomo kwa manufaa ya watu wake.

- Dr Fransis ametumia muda mwingi kufafanua hoja ya wali wengi. Hakika katika hili napenda kulilaumu bunge hili kwa kutoliangalia hili toka mwanzo

- Walio wachache wamekataa taarifa yao kusomwa na Dr Fransis na hivyo mchungaji Msigwa anawasilisha taarifa hiyo

- Kuhusu Ibara ya kwanza, walio wachache wanapendekeza jina liitwe shirikisho kwa vile wakati zinaungana nchi mbili hizi, zilikuwa huru. Hivyo nchi huru zinapoungana, kinachozaliwa ni shirikisho na si Jamhuri. Hapa anamnukuu Prof Issa Shivji

- Msigwa anasema kuwa shirikisho litaondoa utata unaojitokeza ndani ya muungano uliopo ambao umesababisha kuvunjwa kwa katiba ya jamhuri na serikali zote mbili

- Kuhusu mipaka, wanapendekeza ibaki kama ilivyo kwenye rasimu ispokuwa kila nchi iweke mipaka yake kama ilivyokuwa kabla ya muungano

- Mchungaji Msigwa naona alikuja na desa jingine. Alikuwa anasoma taarifa tofauti na iliyowasilishwa kwa Katibu wa Bunge.

- Msigwa amemaliza kutoa ufafanuzi na Mwenyekiti anasema kuwa wabunge wamenufaika na nukuu mbalimbali ila si ufafanuzi wa sura ya kwanza na ya sita

- KAMATI NAMBA NNE
DR HAMISI KIGWANGALLAH anawasilisha taarifa hiyo kwa niaba ya Mwenyekiti Christopher Ole Sendeka ambaye ameenda kwenye kumbukumbu ya kifo cha Edward Moringe Sokoine huko Monduli

- Hamisi Kigwangallah ameanza kwa kutaja majina ya wajumbe walio wengi

- Dr. Kigwangallah anasema kuwa mjadala unaoendelea umetawaliwa na muundo wa muungano anaeleza jinsi changamoto zilizobainishwa na tume ya katiba mpya

- Kama kuna Member wa UKAWA ajitokeze humu kutueleza ni kwa nini mpaka sasa kamati tisa zimewasilisha, hakuna hata msemaji mmoja mwanamke wa maoni ya wachache. Hii ni aibu kubwa kwa UKAWA kukumbatia mfumo dume. Binafsi kuna wanawake jasiri wengi tu ndani ya UKAWA kama akina Esther Matiko, Lucy Owenya, Halima Mdee, Chiku Abwao nk. Kwa nini wanaendekeza mfumo Dume?

- Lissu ameanza mbwembwe zake. Anamnukuu yuleyule Prof Shivji. Prof Shivji anasema kuwa muungano huu haujawahi kuridhiwa na baraza la wawakilishi

- Lissu pia anamnukuu yuleyule Mwakyembe kama walivyonukuu kamati zilizopita. Mwakyembe amenukuliwa akisema kuwa mfumo wa Serikali tatu ni suluhisho pekee la matatizo ya muungqno uliopo

- Tundu Lissu ananukuu pia maoni ya wahadhili 15 wa chuo kikuu cha DSM ambao walipendekeza muundo wa serikali tatu. Anasema kuwa baadhi ya wahadhiri hao wapo ndani ya bunge na wamepiga kura kukataa shirikisho

- Lissu anauliza kama Hati ya Muungano ipo, halali na je Muungano huu ni halali?