• Latest News

  Thursday, August 7, 2014

  MAONYESHO YA NANENANE KANDA YA ZIWA YAENDELEA


  Maonyesho ya nanenane kanda ya ziwa ambayo yalianza tokea tarehe 1/8/2014 katika viwanja vya NYAMHONGOLO jijini mwanza yanaendela kushika kasi kwa muonekano mzuri ni baaada ya bidhaa mbalimbali kuonyeshwa na halmashauri mbalimbali kutoka mikoa yote sita ambayo inaunda kanda ya ziwa ambayo ni MWANZA, SHINYANGA, KAGERA, SIMIYU, GEITA, NA MARA.
  Kwa ujumla maonyesho ni mazuri kwani yamehusisha shughuli nyingi za kilimo na mifugo kama kauli mbiu inavyosema MATOKEO MAKUBWA SASA KILIMO NI BIASHARA.
  Pia kumekua na wajasiriamali wengi sana ambao wamekuja na bidhaa mbalimali zikiwemo bidhaa za ngozi, mikoba, viungo, asali, vyakula vya asili, mashine ndogondogo na vingine vingi vya kuvutia
  Maonyesho ya mwaka huu yamekua tofauti na mwaka jana kwani mwaka huu kila siku kuna kuwa na mgeni rasmi ambaye ni moja kati ya wakuu wa mikoa kutoka katika mikoa husika hii imeongeza maandalizi kuwa makubwa na mazuri zaidi.
  Tazama baadhi ya picha kutoka katika viwanja vya nanenane mwanza

  MAHARAGE YAKIWA SHAMBANI

  MBUZI WA MAZIWA WA KISASA


  MAHINDI PIA YAPO
  WATER BUFFALO  KABICHI KATKIA BUSTANI NDOGO

  NG'OMBE DUME AINA YA BORANI

  SEHEMU YA KUFUGIA VIFARANGA VYA KUKU (BRODER)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MAONYESHO YA NANENANE KANDA YA ZIWA YAENDELEA Rating: 5 Reviewed By: Kilimo mifugo
  Scroll to Top