• Latest News

  Sunday, September 28, 2014

  MAADHIMISHO YA SIKU YA KICHAA CHA MBWA DUNIANI YAFANYWA KWA VITENDO KAHAMA MJINI

  Na Mathias Kavishe
  Siku ya kichaa cha mbwa duniani huadhimishwa kila mwaka tarehe 28 September.
  katika kuadhimishwa kwa siku hiyo duniani halmashauri ya mji wa kahama ikishirikiana na shirika lisilo la kiserikali TAPO (tanzania animal protection) wameadhimisha siku hiyo kwa vitendo ikiwemo kutoa chanjo ya kichaa cha mbwa kwa wananchi wa mji wa kahama na vitongoji vyake bure bila kutozwa kwa gharama yeyote.
  Katika maadhimisho hayo ambayo yalifanyika katika viwanja vya magereza vilivyopo katiaka mji wa kahama Pia walitoa elimu juu ya ufugaji bora wa mbwa kwa kumjali mbwa kama mifugo mingine ifugwayo.
  Wakazi wa mji wa kahama wameonekana kufurahishwa sana na kitendo hiki cha utoaji wa matibabu na chanjo kwa kila mwaka inapoadhimishwa siku ya kichaa cha mmbwa duniani.
  Nikizungumza na baadhi ya watu waliofika katika kupata huduma hii wameupongeza sana uongozi wa halmashauri ya mji wa kahama na shirika la haki za wanyama TAPO kwa kuwapa huduma hii bila gharama yeyote.

  Pichani ni mtaalamu akimhudumia mbwa

  Mbwa aliyetunzwa vizuri
  Mtaalamu wa mbwa akitoa maelekeza kwa mtoto aliyeleta mbwa kwenye chanjo
  Mtaalamu akiwahudumia mbwa walioletwa na wananchi katika viwanja vya magereza
  wataalamu wakishauriana na na mfugaji juu ya mbwa wake jinsi ya kuwatunza kisasa
  Mbwa aina ya German sherfard

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MAADHIMISHO YA SIKU YA KICHAA CHA MBWA DUNIANI YAFANYWA KWA VITENDO KAHAMA MJINI Rating: 5 Reviewed By: Kilimo mifugo
  Scroll to Top