• Latest News

  Thursday, September 25, 2014

  TANGAZO LA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA NAFASI ZAIDI NI NYINGI

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  OFISI YA RAIS
  SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
  UMMA
  Kumb. Na EA.7/96/01/H/03 25 Septemba, 2014
  TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

  Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
  mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
  na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki,
  pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea
  katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
  Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
  Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 102 za kazi kwa ajili ya Katibu Mkuu
  Wizara ya Maji,

  NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
  i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
  ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
  iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
  katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
  kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili
  kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
  v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
  anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
  watatu wa kuaminika.
  vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
  - Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
  - Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
  - Computer Certificate
  - Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
  - Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
  vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
  ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
  xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 8 Oktoba, 2014
  xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
  xiv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.

  Katibu, AU Secretary,
  Sekretariati ya Ajira katika Public Service Recruitment
  Utumishi wa Umma, Secretariat,
  SLP.63100, P.O.Box 63100
  Dar es Salaam. Dar es Salaam.

  1.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UPIMAJI ARDHI) - (ASSISTANT WATER WORKS TECHNICIAN GEOMETRIC) – NAFASI 25-ZINARUDIWA

  Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
  1.1 MAJUKUMU YA KAZI
   Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aoyesajiliwa ili aweze;
   Kushirikiana na Wahandisi wa Maji na kuwaongoza walengwa katika kuchagua njia za kupitisha bomba kwa ajili ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
   Kupima hali ya kijiografia ya maeneo ya inayokusudiwa kujengwa au yenye miradi ya maji na usafi wa mazingira ili kuwezesha usanifu wa miundo mbinu miradi;
   Kupima uwekaji wa vifaa vya miundo mbinu kwenye ardhi wakati wa ujenzi wa miradi ya maji na usafi wa mazingira;
   Kunakili na kutunza taarifa za upimaji wa ardhi kwa ajili ya miundo mbinu ya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa namna inayokubalika kwa mchoraji wa ramani za usanifu wa miradi kufanya kazi yake kwa unadhifu;kuchora ramani za maeneo ya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa namna zote zinazokubalika kwa ajili ya kuwezesha usanifu wa miundo mbinu ya maji na usafi wa mazingira;
   Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za upimaji ardhi.

  1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana Cheti cha ufundi Daraja III (Water Works Technician Geometric).

  1.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.

  2.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI (PAMPU) – NAFASI 25-ZINARUDIWA
  Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

  2.1 MAJUKUMU YA KAZI
   Atafanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili aweze;
   Kufunga pampu na injini za aina mbalimbali za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
   Kufanya usafi na ukaguzi wa pampu na injini za miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
   Kuhudumia uendeshaji wa pampu na injini za miradi ya maji;
   Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na ya kuzuia uharibifu wa pampu na injini kwa kufuata miongozo ya uendeshaji na matengenezo na inapohitajika kwa dharura;
   Kunakiri, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya pampu na injini za miradi ya maji;
   Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.

  2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana Cheti cha ufundi Daraja III (Mitambo Ya Maji (Pampu).

  2.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.

  1.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI (UMEME) – NAFASI 25-ZINARUDIWA
  Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

  1.1 MAJUKUMU YA KAZI
   Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi sanifu aliyesajiliwa ili aweze;
   Kufunga mfumo wa umeme unaohitajika kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
   Kufunga mota na vifaa vingine vya umeme vya aina mbalimbali vya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
   Kufanya usafi na ukaguzi wa mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine umeme vya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu wa pampu na kuzuia uharibifu;
   Kuendesha mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
   Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na ya kuzuia uharibifu kwenye mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine umeme kwa kufuata miongozo ya uendeshaji, na inapohitajika kwa dharura.
   Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
   Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.

  1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana Cheti cha ufundi Daraja III (Plants Technician Electrical).

  1.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.

  3.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI - (ASSISTANT TECHNICIAN WELDING) NAFASI 2-ZINARUDIWA
  Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

  1.4 MAJUKUMU YA KAZI
   Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili aweze;
   Kufunga pampu na injini za aina mbalimbali za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
   Kufanya usafi na ukaguzi wa pampu na injini za miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
   Kuhudumia uendeshaji wa pampu na injini za miradi ya maji;
   Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi nay a kuzuia uharibifu wa pampu na injini kwa kufuata miongozo ya uendeshaji na matengenezo na inapohitajika kwa dharura;
   Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya pampu na injini za miradi ya maji;
   Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.

  1.5 SIFA ZA MWOMBAJI
   Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana Cheti cha ufundi Daraja III katika fani ya Welding na fiter turner.

  1.6 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.

  4.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UFUNDI BOMBA) - (ASSISTANT WATER WORKS TECHNICIAN PLUMBING) – NAFASI 1-INARUDIWA
  Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
  1.7 MAJUKUMU YA KAZI
   Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili aweze;
   Kufunga mitandao ya bomba za aina mbalimbali ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
   Kufanya usafi na ukaguzi wa mitandao ya bomba ya miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
   Kuwezesha uzalishaji na usambazaji wa maji na utoaji wa majitaka kwa kupitia mitandao ya bomba za miradi ya maji na usafi wa mazingira.
   Kufanya matengenezo ya kawaida ya vipindi nay a kuzuia uharibifu wa mitandao ya bomba kwa kufuata ratiba na inapohitajika kwa dharura.
   Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na matengenezo ya mitandao ya bomba za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
   Kumsaidia Fundisanifu kazi za kiufundi.

  1.8 SIFA ZA MWOMBAJI
   Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao wana Cheti cha ufundi Daraja III (Plumbing).

  1.9 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.

  5.0 MHANDISI DARAJA LA II (MAJI) – WATER RESOURCE ENGINEER –
  NAFASI 14-INARUDIWA
  Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

  5.1 MAJUKUMU YA KAZI
   Kushughulikia upembuzi yakinifu, usanifu wa ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu midogo midogo ya usambazaji maji na kushiriki shughuli za upembuzi yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu mikubwa ya ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira.
   Kufanyia mapitio taarifa za upembuzi yakinifu na sanifu za ujenzi wa miundombinu ya miradi ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.
   Kufanyia ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na utengenezaji wa miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kupata ubora unaokusudiwa.
   Kushiriki katika kazi ya kupendekeza miradi na kupitia mapendekezo ya miradi (project proposal) ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.
   Kufanya uchunguzi kuhusu uharibifu wa miundombinu au ajali zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira.
   Kutayarisha bajeti ya utekelezaji wa shughuli za sekta za maji.
   Kusimamia kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo ya miundombinu ya miradi ya maji na usafi wa mazingira.
   Kukusanya na kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za sekta ya maji kwa ajili ya matumizi ya sekta na kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya Wahandisi.

  5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya uhandisi wa Maji (Water Resource Engineering) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

  5.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.

  6.0 MHANDISI DARAJA LA II (MAJI) – WATER RESOURCE WITH GIS ENGINEER – NAFASI 4-INARUDIWA
  Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

  6.1 MAJUKUMU YA KAZI
   Kushughulikia upembuzi yakinifu, usanifu wa ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu midogo midogo ya usambazaji maji na kushiriki shughuli za upembuzi yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu mikubwa ya ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira.
   Kufanyia mapitio taarifa za upembuzi yakinifu na sanifu za ujenzi wa miundombinu ya miradi ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.
   Kufanyia ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na utengenezaji wa miundombinu ya uzalishaji na usambazaji maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kupata ubora unaokusudiwa.
   Kushiriki katika kazi ya kupendekeza miradi na kupitia mapendekezo ya miradi (project proposal) ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.
   Kufanya uchunguzi kuhusu uharibifu wa miundombinu au ajali zinazojitokeza wakati wa utekelezaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira.
   Kutayarisha bajeti ya utekelezaji wa shughuli za sekta za maji.
   Kusimamia kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo ya miundombinu ya miradi ya maji na usafi wa mazingira.
   Kukusanya na kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za sekta ya maji kwa ajili ya matumizi ya sekta na kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya Wahandisi.

  6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya uhandisi wa Maji (Water Resource with GIS) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.

  6.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.

  7.0 MHANDISI KILIMO DARAJA LA II (AGRO – ENGINEERS) – NAFASI 6-INARUDIWA
  7.1 MAJUKUMU YA KAZI
   Kuandaa program za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo,
   Kushiriki katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana,
   Kushiriki kutengeneza michoro/ramani za umwagiliaji,
   Kushiriki katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji,
   Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafunindisha wakulima uendeshaji wa skimu za umwagiliaji,
   Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji,
   Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji pamoja na matumizi ya maji,
   Kuandaa mafunzo/maonyesho ya matumizi ya za za kilimo,
   Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta,
   Kuwafundisha wakulima ujenzi wa vihengo bora na
   Kushughulikia ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji ipasavyo.

  7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
   Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (Bachelor Degree) ya uhandisi yenye mwelekeo mkubwa katika fani ya Kilimo cha umwagiliaji na cha zana kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.
  7.3 MSHAHARA
   Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS E Kwa mwezi.
  X.M. DAUDI
  Katibu
  Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: TANGAZO LA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA NAFASI ZAIDI NI NYINGI Rating: 5 Reviewed By: Kilimo mifugo
  Scroll to Top