• Latest News

  Monday, September 15, 2014

  UPASUAJI-MATIBABU YA NGOME ALIYEKULA MAKARATASI NA MIFUKO YA RAMBO KWA NJIA YA UPASUAJI
  Na mathias kavishe
  Madaktari wa halmashauri ya mji wa Kahama waendelea kutoa huduma bora kwa wafugaji hasa za matibabu kwa wale mifugo  wagonjwa na ushauri juu ya kufuga kwa kitaalamu ili kupata mavuno bora yatokanayo na mifugo.
  Tukiongea na baadhi ya wananchi wa mji wa Kahama wanasema kua madaktari  wa mifugo katika mji huu wamekua wakifanya kazi yao kwa moyo licha ya changamoto mbalimbali ambazo wamekua wakikabiliana nazo.

  Katika hali ya kufurahisha kamera yetu iliwakuta wakifanya “operation” upasuaji kwa ngombe aliyekua amekula makaratasi na mifuko mingi ya Rambo iliyokua imejaa tumboni na kumfanya ngombe kushindwa kupata afya nzuri na wakati mwingine kumfanya ahisi maumivu ya tumbo.  Wataalamu wakishirikiana katika upasuaji DR. DAMIANI, DR. KIJA AND DR. MKURATI

  Baada ya mahojiano marefu na madaktari hao walieleza mtandao wetu kuwa wamekua wakitoa huduma ya upasuaji kwa mifugo mingi wenye tatizo kama hilo na wamepona kabisa.
  Pia wameelezea kumekua na changamoto nyingi katika sekta ya mifugo mjini Kahama na mkoa wa shinyanga kwa ujumla kwa kutokua na maabara ya utafiti na vipimo vya magonjwa ya mifugo hali inayochangia kufanya kazi katika mazingira magumu hasa pale tunapotakiwa kutoa huduma bora ya matibabu kwa wafugaji. Hayo yameelezwa na daktari wa halmashauri wa mji wa Kahama wakati akifanya operation hiyo kwa mfugaji mmoja.

  Pamoja na mazingira ya kazi kuwa magumu wanajitahidi kufanya kazi kwa moyo na nguvu kadri wawezavyo ili kufanikisha malengo ya wafugaji na bila kuwakatisha tamaa alisema daktari huyo.


  Wataalamu wakijadiliana jambo

  Wakisafisha kabla ya kushona kidonda
  dr. damiani akiendelea na usafi wa sehemu iliyopasuliwa
  Dr. kija akishona sehemu ya ndani ya tumbo la ngombe
  Ushonaji unaendelea hadi kuhakikisha sehemu yote ya ndani imefunga vizuri
  Dr. damian akiendelea na ushonaji


  Huu nu muonekano baada ya kushona sehemu ya ndani inafuata sehemu ya kati na ya juu ambayo ni ngozi
  Wakishona sehemu ya juu ya ngozi

  Dr. damiani akikaza uzi baada ya kushona sehemu ya juu ya ngozi

  Baada ya kushona na mnyama anaendelea vizuri
  Wataalau wakiosha sehemu ya juu ili kumuacha mnyama katika hali ya usafi

  Mr. kavishe na Mr. mkurati wakijadiliana jambo Baada ya kuoshwa vizuri anapuliziwa wound spray kwa ajili ya kutunza kidonda vizuri pia kuzuia inzi wengi kutua pale

  Dr. kija akinmwekea dawa katika kidonda.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: UPASUAJI-MATIBABU YA NGOME ALIYEKULA MAKARATASI NA MIFUKO YA RAMBO KWA NJIA YA UPASUAJI Rating: 5 Reviewed By: Kilimo mifugo
  Scroll to Top