• Latest News

  Thursday, October 9, 2014

  JINSI YA KUMTUNZA PUNDA VIZURI KWA KAZI NZURI


  NIRA KWA PUNDA
  PUNDA MWEMA KAZI NJEMA

  Utangulizi
  Wanyama kazi ni wanyama wasaidiao katika shughuliza kila siku za mwanadamu kama vile kilimo,usafiri,na shughuli zinginezo nyingi.
  Miongoni mwa wanyama hao ni kama vile Ng’ombe, punda, farasi, ngamia na mbogo maji.
  Kwa kawaida wanyama hawa hufanya kazi kulingana na maumbile yao mfano ng’ombe hufanya kazi kwa kutumia shingo yake ambayo hufungwa Nira, Farasi , Punda Ngamia hufanya kazi kwa kupitia kifua chao ambao hutumia mikanda na hatamu.

  PUNDA
  Huyu ni mnyama afugwae na binadamu na hutumika katika za binadamu. Mnyama huyu hutumia nguvu kifuani na kupeleka kwenye zana, mkanda huitwa mikanda ya punda. ( Donkey Chest Harnessing Belts) ambapo mikanda hiyo ina viambatanisho vifuatavyo:-
  • Brode – mikanda ya kichwani
  • Breast band – mkanda wa kifuani
  • Back strap – mkanda wa mgongoni
  • Breaking strap – mkanda wa kizuizi

  Mikanda hii kwa pamoja huambatana na viambatanisho vifuatanyo:-
  • Kigogo – saddle
  • Gunia – sack
  • Gurudumu la mgongo – back  KUMFUNDISHA PUNDA
  Kwa kawaida mnyama huyu mafunzo yake huchukua muda wa siku 7 – 14 hadi kujua, kuna njia mbili za mafunzo ambazo ni njia ya ti mu na njia ya awali.
  Njia ya timu hujumuisha punda wawili hadi wanne ambao huunganishwa kwa punda wanaojua na wasiojua mafunzo ,wanaojua hukaa mbele ya wasiojua.
  Njia ya awali hutumika kumfunza punda mmoja kwa kupewa amri tofauti mfano panda kulia, panda kushoto, simama fuata kushoto nk.
  Umri wa kumfunza punda ni kuanzia mwaka mmoja na nusu hadi miaka miwili.


  Mbembeleze punda akuzoee
  Punda ni rafiki mwema   Punda hawa hufanya kazi siku nzima wanaonekana kuchoka sana  Punda aliyeelemewa na mzigo


  RATIBA YA KAZI
  • Kuamka na kuchunga nia kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 1 asubuhi
  • Kufanya kazi ni kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 4 asubuhi
  • Mapumziko na lishe ni kuanzia saa 5 asubuhi hadi saa 10 jioni
  • Kufanya kazi jioni ni kuanzia saa 11 jioni hadi saa 12 jioni
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: JINSI YA KUMTUNZA PUNDA VIZURI KWA KAZI NZURI Rating: 5 Reviewed By: Kilimo mifugo
  Scroll to Top