• Latest News

  Monday, October 20, 2014

  MAKALA: JE! WATANZANIA WANANUFAIKA NA RASILIMALI ZA NCHI YAO HUSUSANI MADINI?


        

  SEHEMU YA KWANZA

  UTANGULIZI
  Tanzania ni moja kati ya nchi chache duniani ambazo zimebahatika kuzungukwa na migodi ya aina mbalimbali na madini ya aina mbalimbali .

      Ukijaribu kuzunguka Tanzania katika kila kanda ya nchi hii utasikia  habari kuwa kuna machimbo na migodi mikubwa .Hii ni kutokana na na utajiri mkubwa tuliobahatika kupewa na Mwenyezi mungu ambao hatuna budi kujivunia kwa kweli pia kumshukuru mungu kwa yote hayo.
  Pia inabidi tuendelee kumshukuru Mungu sana kwa kutuwezesha kuwepo katika nchi kama hii maana kuna nchi ukizunguka nchi nzima utaishia kuambiwa kuna kamgodi kamoja tu tena hakana rasilimali za kutosha sanasana utaambiwa ni makaa ya mawe tena uzalishaji wake ukiwa mdogo sana.
           Katika utafiti uliofanyika kupitia mtandao wetu umebaini kuwa Tanzania tumebahatika kuwa na madini ya aina mbalimbali tena ya thamani kubwa sana yakiwemo TANZANITE ambayo yanapatiakana Tanzania peke yake kule MERERANI arusha ,Pia tunaongoza kuwa na migodi mikubwa ya dhahabu kama vile BUZWAGI NA BULIANG’HULU ambayo inapatikana mkoani shinyanga wilaya ya Kahama . Vilevile migodi ya MWADUI ambayo pia inapatikana Shinyanga, pamoja na migodi ya GEITA GOLD MINING ambayo hupatiakana mkoani geita.

           Ukiachilia mbali hayo yote usisahau kuitaja migodi ya makaa ya Mawe kule mbeya ambapo uzalishaji wake ni mkubwa tu . tukiendelea kubakia kanda ya ziwa tunakutana na migodi mingine kule mkoani mara ambayo ni maarufu kwa uzalishaji wa dhahabu pia ijulikanayo kama NORTH MARA GOLD MINNIG
     Vilevile hutosita kutaja mkoa wa Ruvuma kule wilaya ya tunduru ambapo utakutana na migodi mingine mikubwa ambapo ukizungika mji mzima wa tunduru hutoacha kukutana na viofisi vidogovidogo vingi vya ununuzi wa madini ya aina mbalimbali. Pia migodi ya KIWIRA KULE NZEGA, na mingine mingi ambayo ipo kuizunguka nchi yetu nzuri Tanzania.
  Tukiachana na hiyo migodi mikubwa pia kuna machimbo madogo madogo ambayo yametapakaa katika kila kona ya nchi yetu.
  Kwa utafiti inaonyesha kuwa ukizungumzia wachimbaji wadogo wadogo ni wengi sana katika hii nchi yetu kama vile kule chunya mbeya, geita, nzega, n.k hasa ukuzungumzia wilaya Kahama imezungukwa na wachimbaji wadogo wadogo wengi sana hadi kufikia sehemu Kahama inajulikana mitaani kwa jina la GOLD CITY .
  Moja wapo wa machimbo hayo ni kama vile:-
  Mwime, mwabomba 1, 2, 3, Mwakitolyo 1, 2, 3 , 4, 5, Mwazimba  na mingine mingi maana hiyo ni baadhi tu kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu. Pamoja na hayo bado watu wanaendelea kugundua vijimachimbo vidogovidogo vingi tu kila kukicha.hiyo ni wilaya moja tu ya Kahama kwa Tanzania nzima kuna machimbo madogo madogo mengi sana karibia au zaidi ya elfu moja kwa kuwa karibia kila kona ya nchi kila mtua anajaribu kuchimba kile anachokiona kinamfaa yeye kama mchimbaji.
            Tukiachilia mbali hayo ya migodi na machimbo kwa neema ya pekee nchi yetu imebahatika kuwa na uvunaji mwingine mkubwa wa gesi asilia ambayo sasa hivi kila chombo cha habari lazima kipate kuongelea juu ya gesi hiyo iliyopo huko mkoani MTWARA ambapo hata uvunaji wake haujaanza kikamilifu.

     Pia utafiti wa mafuta ambao unaendelea katika ardhi ya Tanzania hakika ni neema ya pekee ambayo naweza kusema watanzania tumepewa na mwenyezi mungu kwa maaana tukianza kutaja rasilimali tulizonazo tukijumuisha na mbuga nyingi za wanyama ambazo zinavutia sana, mlima Kilimanjaro, ngorongoro cretor, na sehemu za vivutio kama vile Amboni Tanga,Kimindo cha mbeya, Imillah historical sites, na nyingine nyingi ambazo kama tutaanza kutaja twaweza kujaza mia mia bila hata kuzimaliza.
  Itaendelea ; endelea kufuatilia makala hii  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: MAKALA: JE! WATANZANIA WANANUFAIKA NA RASILIMALI ZA NCHI YAO HUSUSANI MADINI? Rating: 5 Reviewed By: Kilimo mifugo
  Scroll to Top