• Latest News

  Wednesday, November 26, 2014

  SOMA MAJINA YA WALIOKULA FEDHA ZA AKAUNTI YA ESCROW KATIKA RIPOTI YA PAC INAYOSOMWA SASA BUNGENI.


  Zitto: Upande wa viongozi wa kisiasa ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; Mhe. Andrew Chenge (Mb)
  Zitto: Andrew Chenge aliingiziwa shilingi bilioni 1.6.
  Zitto: Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa 62 Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6.
  Zitto: Mhe.William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4
  Zitto: Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini alipewa shilingi milioni 40.4.
  Zitto: Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga alipewa shilingi milioni 40.4
  Zitto: Dr. Enos S. Bukuku ambaye alikuwa Mjumbe wa Bodi ya TANESCO aliingiziwa shilingi milioni 161.7.
  Zitto: Upande wa Majaji Prof. Eudes Ruhangisa, aliingiziwa milioni 404.25 na J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4
  Zitto: kwa upande wa Watumishi wa umma,Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa shilingi milioni 40.4
  Zitto: Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4
  Zitto: Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8.
  Zitto: Viongozi wa Madhehebu ya Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni Askofu 63 Methodius Kilaini shilingi 80.9
  Zitto: Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4 na Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4.
  Zitto: Watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, mabox, magunia na lumbesa TegetaEscrow
  Zitto: Bilioni 73.5 zilitolewa na kugawanywa kwa watu mbalimbali kinyume cha Sheria ya Benki Kuu na Taasisi za Fedha ya 2006
  Zitto: Taarifa ya benki (bank statements) yenye majina na akaunti zote zilizoingiziwa fedha zimeambatishwa.
  Zitto: Kamati imebaini mawasiliano kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: SOMA MAJINA YA WALIOKULA FEDHA ZA AKAUNTI YA ESCROW KATIKA RIPOTI YA PAC INAYOSOMWA SASA BUNGENI. Rating: 5 Reviewed By: Kilimo mifugo
  Scroll to Top