Panda kwa nafasi zilizopendekezwa na wataalamu. Kumbuka kuwa na idadi ya mimea inayopendekezwa shambani ni chanzo cha mavuno mengi kwani wingi wa mimea unamaanisha wingi wa wazazi shambani.
Panda kwa msitari ili kurahisisha zoezi la palizi, utiaji mbolea na uvunaji.
Nafasi zitumikazo kupanda mpunga shambani.
Nafasi kati ya shina na shina (Sm)
Idadi ya mimea katika Ekari
Idadi ya mimea katika Hekta
20 kwa 20100,000250,000
15 kwa 15177,778444,444
15 kwa 20133,333333,333
25 kwa 2564,000160,000
25 kwa 2080,000200,000


Hata hivyo, uchaguzi wa vipimo vya kutumia shambani hutegemea:
a.Aina ya mbegu, ndefu-mbali mbali, fupi – karibu karibu

b.Rutuba ya shamba, rutuba nyingi – karibu karibu, rutuba kidogo – mbali mbali