• Latest News

  Sunday, March 29, 2015

  JE WAJUA KILIMO CHA NYANYA KWENYE BANDA NA FAIDA ZAKE(GREEN HOUSE)

  tomato

  Je Wajua Kilimo cha Nyanya kwenye Banda-kitalu

  Darius Cheruiyot
  Kama ilivyo kwa vijana wengi wanaohangaikia maisha, Darius Cheruiyot wa Silibwet, Tarafa ya Bomet, amejaribu kushindana na maisha kwa njia nyingi, amejaribu ufundi makanika, udereva hadi kuwa dereva wa bodaboda. Huko kote hakukumfanikisha kimaisha hadi alipojishughulisha na kilimo. Darius (36) mkulima wa nyanya anapenda kuwashirikisha kwenye kilimo cha nyanya kwa kutumia banda kitalu (green-house). “ Wazo la kuanzisha banda kitalu ili kulima nyanya liliibuka mwaka 2012 baada ya kutembelea shamba la binamu yangu. Nilivutika sana na kile nilichokiona.” Cheriiyot alibainisha. Aliamua kulima kwa kilimo cha banda kitalu kwani alikuwa amejaribu kulima nyanya kwenye eneo la wazi; alipata hasara kwa kuwa nyanya zilishambuliwa na magonjwa na wadudu waharibifu.
  Ili ajenge Banda kitalu ilimbidi kuuza pikipiki yake kwa Sh.55,000 ( sawa na Sh. 990,000 za Tanzania). Familia yangu ikaniongezea Sh. 25,000/- (sawa na Sh. 450,000/ za Tanzania) ambazo nilizitumia kujenga Banda kitalu. Pia nilinunua polithine na mabomba ambayo niliyatumia kwenye mradi huu.” Alisema Cheruiyot.
  Nilifanikiwa kujenga baada ya kupata maelekezo na vipimo toka kwenye ofisi ya kilimo. Alijenga banda kitalu la ukubwa wa 17m kwa 13m lililoweza kupandwa miche/ mashina 1,200. Mapema mnamo mwaka 2013, na hakufanikiwa sana kwa kuwa yalikuwa mazao yake ya kwanza. Hakutaka kuangalia nyuma kwani alijua ingemvunja moyo. “ Sikupanda kwa kuzingatia nafasi, miti ilirefuka lakini haikuzaa nyanya za kutosha. Aidha, nikagundua kwamba nilikuwa natumia kiasi kikubwa cha mbolea, hili lilinikamua kiuchumi, ilibidi nifanye jambo hapo.”
  Na kabla sijapanda awamu iliyofuata, alihakikisha anatumia samadi kutoka kwenye mifugo ya familia yao. Alitumia samadi ya ng’ombe akaichanganya na udongo wa bandakitalu kabla ya kupanda nyanya. “Mboji ilinisaidia kupunguza matumizi ya mbolea ya viwandani , nilitumia majani makavu kila baada ya majuma mawili”.
  Cheruiyot anasema alipata takribani Sh. 200,000/- (sawa na Sh.3,600,000/- za Tanzania) kwa miezi mine ya mavuno ya nyanya zake. Anavuna nyanya kila baada ya siku mbili, na anauza sanduku / kreti moja la nyanya kati ya Sh. 500 hadi Sh. 2,000/- (TSh.9,000 hadi 3,600/- )Wengi wa wateja wake huja kununua nyumbani kwake na huenda kuzilangua katika masoko ya Bomet, Libwet na Tenwek.
  Wakulima ambao wanapenda kujishughulisha na mradi kama huu kwa faida, hawana budi kuwa na ujuzi fulani. “Kwanza, nyanya zinataka eneo la joto na jua, zinahitaji angalau masaa 8 ya kupata jua kila siku, zikikosa jua huzaa matunda machache. Udongo unahitaji uwe na pH 5.5 hadi 6.8, wenye maji ya kutosha na ulio na rutuba ya kutosha.
  Cheriuyot anasema,”’Mbinu nyingine ni kwamba anatumia mkojo wa sungura kwenye mche wa nyanya kabla nyanya hazijatoa maua. Mkojo wa sungura unasaidia kuzuia wadudu na kusaidia kuotesha nyanya.”
  Kila mradi wa kilimo unapoanzishwa haukosi changamoto. Awali, miche yake ilikauka mara tu ilipotoka kupandwa.
  Via standardmedia.co.ke
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: JE WAJUA KILIMO CHA NYANYA KWENYE BANDA NA FAIDA ZAKE(GREEN HOUSE) Rating: 5 Reviewed By: Kilimo mifugo
  Scroll to Top