• Latest News

  Monday, August 10, 2015

  Ng'ombe 'waandamana' kupinga bei duni ya Maziwa

  Kutoka bbc news

  Mshirikishe mwenzako

  Ng'ombe 'waandamana' kupinga bei duni ya Maziwa Uingereza

  Ushawahi kukutana na ngo'mbe katika maduka ya jumla?
  Na ushawahi kusikia maandamano yanayojumuisha ng'ombe ?
  Amini usiamini wanunuzi katika maduka ya kifahari katika mji ya Asda Queensway, Stafford Uingereza walipigwa na butwaa ng'ombe walipoingia dukani humo !
  Yamkini mifugo hao waliletwa humo na wakulima waliokuwa wakiandamana kupinga bei duni ya maziwa wanaoyolipwa na uongozi wa maduka hayo ya jumla.
  Wakulima 70 wakiandamana na ng'ombe wawili walishiriki katika maandamano hayo ya kipekee.
  Mnunuzi mmoja Adam Williams aliiambia BBC kuwa hata wahudumu wa duka hilo hawakuficha mshangao uliowakumba.
  Walipigwa na butwaa wote ng'ombe walipoingia dukani!''
  Walisababisha hali ya mshikemshike kwani walifululiza hadi upande wa ndani kabisa ya duka hilo!''
  Wakulima hao wanataka maduka hayo ya jumla yawaongezee bei ya maziwa ili na wao waweze kujikimu kimaisha.
  Hata hivyo wasimamizi wa maduka hayo ya jumla wanasema kuwa hilo halitafanyika.

  Wakulima 70 waliandamana na ng'ombe wawili

  Wanadai kuwa hakuna uhusiano wowote wa bei ya juu ya maziwa katika maduka yao na bei duni wanayolipwa wakulima shambani.
  Mkulima mmoja kutoka Stafford Matthew Weaver, amenukuliwa akisema
  "Tulijua kuwa iwapo tunataka kupata ufanisi katika maandamano yetu ilikuwa lazima tufanye kitu cha kipekee ambacho pia kitawavutia watu na kuwapa sababu ya kuwachekesha.''
  Weaver alisema wafugaji hao walitokea Derbyshire, Shropshire na Warwickshire .
  Alisema kuwa bado wanapanga maandamano mengine katika maduka zaidi.
  Kampuni ya maziwa ya Muller ilitangaza kuwa itapunguza bei ya maziwa kwa sababu soko lake limeporomoka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: Ng'ombe 'waandamana' kupinga bei duni ya Maziwa Rating: 5 Reviewed By: Kilimo mifugo
  Scroll to Top