• Latest News

  Wednesday, June 1, 2016

  Kilimo Bora cha Zabibu


  Zabibu

  Shamba la mizabibu
  Zabibu ni tunda la mzabibu (Vitis vinifera).
  Zabibu moja ni fuu inakua pamoja na fuu nyingine 6 - 300 kwenye mshikano au shazi kama ndizi. Zabibu hupatikana kwa rangi mbalimbali hasa kijani, njano, buluu, nyeusi na namna za nyekundu.
  Zabibu zinajulikana hasa kama chanzo cha divai lakini huliwa kama tunda, hufanywa kuwa maji ya zabibu, kuwa jem au kukaushwa kuwa zabibu kavu. Mbegu zake ndogo hutoa mafuta.
  Table grapes on white.jpg

  Utangulizi[hariri | hariri chanzo]

  Mzabibu ni mmea wa jinasi ya "Vitis"; uliokuwa muhimu katika mabadiliko ya maisha ya mwanadamu, kitaalamu tunda dogo, linalolimwa kwa miaka zaidi na kupukutisha majani. Zabibu huweza kuliwa mbichi au zikatumika kutengenezea jemu, sharubati, jeli, siki, madawa, mvinyo, zabibu kavu na mafuta ya mbegu zake. Zabibu pia hutumika kutengenezea vitu vitamu vitamu. Zabibu wakati mwingine hutumika kama alama ya dhamiri.

  Historia[hariri | hariri chanzo]

  Kilimo cha zabibu kilianza mahali kunapofahamika sasa kama Uturuki. Hamira, moja ya viumbe wadogo waliofahamika mapema zaidi, hupatikana kiasili kwenye ngozi ya zabibu, na kupelekea kugunduliwa kwa vileo kama vile mvinyo. Kumbukumbu za kihistoria za huko Misri zinaonesha kilimo cha zabibu, na hata zamani ya Ugiriki, Foenesia na Roma pia walilima zabibu kwaajili ya kula na kutengeneza mvinyo. Baadae, kilimo cha zabibu kilisambaa mpaka Ulaya, kaskazini mwa Afrika, na hatimaye mpaka Amerika ya kaskazini.
  Zabibu za asili ni zile za jenasi ya "vitis" iliyoenea upesi maeneo ya Amerika ya kaskazini, na ilikuwa sehemu ya mlo kwa watu wengi wa mwanzo wa Amerika ya kaskazini, lakini ilionwa na wakoloni kutoka Uingereza kuwa hazifai kwa kutengeneza mvinyo. Zabibu za Dunia ya Kale, vitis vinifera zililimwa huko Calfornia ambako Hispania walianzisha msululu wa monasteri kwenye fukwe kwaajili ya wanajeshi wao na machungwa tele kuwakinga na ugonjwa na ngozi kiseyeye na kwabadilisha wazawa.

  Maelezo[hariri | hariri chanzo]

  Zabibu hukua kwenye kichana chenye zabibu 6 mpaka 300, na huweza kuwa za rangi nyekundu iliyoiva, nyeusi, bluu ya kukoza, njano, kijani na hata pinki. Zabibu “nyeupe” huwa na rangi ya kijani hasa, na kiasili hutokana na zabibu nyekundu. Kubadilika hukukwa kizazi hutokana na zabibu kukata uzalishaji wa pigmenti ya anthocyanins ambazo huwa na jukumu la kuzipa rangi zabibu. Pigmenti hii ya anthocyanins na nyingine kadhaa za familia ya ‘polyphenols’ kwenye zabibu nyekundu na huhusika na kubadilisha kivuli kwenye mvinyo mwekundu.

  Mizabibu[hariri | hariri chanzo]

  Grapes Angoor.JPG
  Zabibu nyingi hutokana na mazao ya "Vitis vinifera", zabibu ya Ulaya yenye asili ya Mediterania na Asia ya kati. Kiasi kidogo cha zabibu na mvinyo hutokana na spishi za Amerika na Asia. Vitis labrusca, sharubati ya mezani na mizabibu ya huko Amerika ya Kaskazini ( hujumuisha aina kali ), na wakati mwingine hutengenezea mvinyo. Asili yake ni Marekani mashariki na Kanada. Vitis riparia, mzabibu mwitu wa Amerika ya kaskazini, wakati mwingine hutumika kutengenezea mvinyo na jemu. Asili yake ni Marekani mashariki na Kubeki kaskazini. "Vitis rotundofolia", hutumika kwa mvinyo na jemu. Asili yake ni Marekani kusini-mashariki kutoka Deleware mpaka Ghuba ya Mexico. Vitis amurensis, spishi muhimu ya Asia.

  Mgawanyiko na uzalishaji[hariri | hariri chanzo]

  Kulingana na shirika la Umoja wa mataifa la chakula na kilimo, ( FAO ), kilometa za mraba za dunia zinatumika kwa kilimo cha zabibu. Asilimia 71 ya zabibu yote duniani hutumika kutengeneza mvinyo, 27% huliwa kama matunda ya kawaida na 2% kama zabibu za kukausha. Maeneo haya yaliyotengwa kwa kilimo cha zabibu hukua kwa 2% kila mwaka. Jedwali lifuatalo linaonesha wazalishaji wakubwa wa mvyinyo na maeneo ya nchi hizo yaliyotengwa kwa kilimo cha zabibu.

  Zabibu zisizo na mbegu[hariri | hariri chanzo]

  Kutokuwa na mbegu ni ubora wa zabibu unaohitajika katika uchaguzi wa zabibu, na zabibu zisizo na mbegu sasa huchukua asilimia kubwa ya zabibu kwaajili ya kuliwa na watu. Kwasababu mizabibu hupandwa kwa vipandikizi, kukosekana kwa mbegu hakuna matatizo yeyoye kwa wakulima. Huwa tatizo tu kwa wakulima ambao wanataka aidha kutumia mbegu kuhifadhi kizazi husika au kama wanataka kufanya mabadiliko katika hatua za mwanzo za kiini kwa kutumia tishu kwa kutumia mbinu za ukuzaji wa bakteria.
  Kuna vyanzo kadhaa vya zabibu zisizo na mbegu, na kimsingi mazao yote ya kibiashara yametokana na vyanzo vikuu vitatu: Thompson Seedless, Russian Seedless, na Black Monukka, aina zote hizi zikiwa ni za spishi ya Vitis vinifera. Hivi sasa kuna zabibu zisizo na mbegu nyingi kiasi, kama vile Einset Seedless, Reliance na Venus, zimekuwa zikilimwa kwa ajili ya ugumu na kwa wastani kuwa baridi kwenye maeneo ya baridi ya kaskazini mashariki ya marekani na kusini mwa Ontario. Fidia ya kuwa na kula zabibu hizi za hali ya juu ni kukosa faida lukuki muhimu zinazotokana na kemikali zenye virutubisho tele zilizopo kwenye mbegu za zabibu.

  Zabibu za kukaushwa[hariri | hariri chanzo]

  Raisins 01.jpg
  Zabibu huliwa pia zikiwa zimekaushwa, kuongeza pia uwezo wa kustahimili kukaa kwa muda mrefu. Huko Ulaya, zabibu za kukaushwa huitwa ‘raisins’ au kwa lugha nyingine za asili. Na huko Uingereza kuna aina tatu za zabibu za kukaushwa na hii ililazimisha mamlaka kutumia msamiati “ mazao ya kukaushwa ya mzabibu” kwenye nyaraka za kiofisi. “Raisin” ni zabibu yeyote ya kukaushwa. Huku neno raisin likiazimwa kutoka kwene lugha ya kifaransa, katika kifaransa neno hili humaanisha zabibu mbichi za kawaida. Kifaransa ‘grape’ (ambapo katika kiingereza huwa ‘grape’ na Kiswahili ‘zabibu’) “Currant” hukaushwa kutokana na zabibu za Zante Black Corinth, jina lilochukuliwa tena kutokana na lugha ya kifaransa, raisin de Corinthe ( zabibu za Corinth ). Tambua pia kuwa Currant imekuja kuwa na maana ya blackcurrant na redcurrant, matunda yasiyohusianan na zabibu kabisa.
  “Sultana” kiasili ni raisin iliyotengenezwa kutokana na aina maalumu ta zabibu kutoka Uturuki, lakini dunia sasa inatumia msamiati huu kumaanisha raisins zilizotengenezwa kwa zabibu za kawaida na kutengenezwa zifanane na sultana ya kweli. Masuala ya Afya.

  Imeandaliwa kwa msaada wa wikipidia

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: Kilimo Bora cha Zabibu Rating: 5 Reviewed By: Kilimo mifugo
  Scroll to Top