• Latest News

  Saturday, June 10, 2017

  ORODHA YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI KWA MWAKA 2017/18

  JUMLA ya wanafunzi 2,999 wamekosa fursa ya kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi kati ya wanafunzi 96,018 waliochaguliwa.
  Hayo yalielezwa leo na Waziri wa Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari juu ya matokeo ya kujiunga na kidato cha tano katika mwaka wa 2017.
  Simbachawene amesema Jumla ya watahiniwa wa shule 349,524 wakiwemo wasichana 178,775 sawa na asilimia 51.1 na wavulana 170,749 sawa na asilimia 48.9 waliofanya mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka 2016.
  Amesema watahiniwa wakujitegemea waliofanya mtiahani huo mwaka 2016 walikuwa 47,751 wakiwemo wasichana 24,587 sawa na asilimia 51.5 na wavulana 23,164 sawa na asilimia 48.5.
  Simbachawene amesema watahiniwa waliofaulu kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa Tanzania Bara.
  Amesema kutokana na hali hiyo ufaulu katika mwaka 2016 uliongezeka kwa asilimia 3.15 ikilinganishwa na na ufaulu wa mwaka 2015.

  KUYAONA MAJINA BOFYA HAPA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: ORODHA YA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO NA VYUO VYA UFUNDI KWA MWAKA 2017/18 Rating: 5 Reviewed By: Kilimo mifugo
  Scroll to Top