• Latest News

  Wednesday, January 24, 2018

  KIWAVI JESHI VAMIZI [Fall Armyworm] MDUDU HATARI KWA ZAO LA MAHINDI


  Kiwavijeshi Vamizi ajulikanae kama Fall Armyworm au kwa jina la kitaalamu “Spodoptera frugipedra” asili yake ni Bara la America. Mdudu alionekana kwa mara ya kwanza katika nchi za Africa Magharibi (Nigeria) mwishoni mwa mwaka 2016
  Hadi mwezi February 2017, kiwavijeshi huyu alikuwa ameshavamia nchi za Afrika Kusini, Kati na Mashariki zikiwemo Zimbabwe, Msumbiji, Zambia, Congo na Rwanda
  Hapa nchini kiwavijeshi vamizi aliripotiwa kwa mara ya kwanza katika wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa mwezi Machi 2017.
  Hadi mwezi Disemba 2017 kiwavijeshi huyu alisharipotiwa kwenye mikoa zaidi ya 15 Maarufu kwa kilimo cha mahindi ikiwemo Mbeya, Shinyanga,Ruvuma, Iringa, Geita, Manyara,Arusha, Kilimanjaro, Morogoro,Tanga, Kigoma, Kagera,Mwanza,Pwani na Lindi.

  Mzunguko wa Maisha ya Kiwavijeshi vamizi {Fall Armyworm}
  Ukuaji wa mdudu huyu hupitia katika hatua nne za ukuaji ambazo ni yai – kiwavi – buu – mdudu kamili (nondo). Hatua ya kiwavi ndiyo inayoshambulia na kuathiri mazao.

  Mazao yanayoshambuliwa na Kiwavijeshi vamizi (Fall Armyworm)

  Kiwavijeshi ( Spodopter frugipedra) hushambulia aina nyingi za Mazao mfano nafaka (Mahindi, Mtama,Mpunga) Mikunde, mbogamboga, (nyanya, mchicha, matikiti, pilipili) ,mbegu za mafuta (karanga, alizeti,pamba) ,miwa, matunda, (migomba, miembe, michungwa) pamoja na malisho ya mifugo mf. Mabingobingo.
  Kiwavijeshi vamizi hushambuliwa mazao katika hatua zote za ukuaji kwa mfano mahindi hushambuliwa yakiwa bado machanga hadi wakati yameshakomaa hivyo kufanya udhibiti kuwa ngumu na wa gharama kubwa.

  Dalili za uharibifu wa Kiwavijeshi Vamizi kwenye zao la Mahindi.
  • ·         Mdudu huyu hufanya uharibifu wa mazao akiwa katika hatua ya kiwavi (lava stage).
  • ·         Hatua ya kwanza ya kiwavi (1st instar) hushambulia majani.
  • ·         Majani ya Mahindi hutobolewa na kuacha matundu makubwa
  • ·         Mabaki ya kinyesi kinachofanana na pumba huonekana juu ya majani ya mahindi
  • ·         Viwavi huonekana kwenye magunzi, shina, na mbelewele  Wadudu wanavyoonekana sehemu ya mmea unapoota


  Mdudu akishambulia kwenye gunzi ka Mhindi
  Jinsi ya Kudhibiti Kiwavijeshi Vamizi (Fall Armyworm)
  Udhibiti wa kibaiolojia

  Matumizi ya viumbe marafiki kama vile Manyingu mf. Telenomus spp, Earwings, na Kuvu mf. Beauvera bassiana ,Bacillus thrugiensis n.k

  Udhibiti Sango
  • ·         Tumia mitego ya kuwanasa nondo ili kubaini mapema uwepo wa kiwavijeshi vamizi
  • ·         Andaa shamba mapema na lima kwa kutifua ardhi ili mabuu (pupae) yaweze kukaushwa na Jua au kuliwa na ndege /wadudu wengine
  • ·         Panda kwa wakati kwa kutumia mbegu na mbolea zilizoshauriwa na wataalamu kwenye eneo lako
  • ·         Zingatia uzafi wa shamba kwa kuondoa magugu nyasi kuzunguka shamba na mabaki ya mazao ya msimu uliopita yanayoweza kuwa na masalia ya wadudu
  • ·         Kagua shamba mara kwa mara n aondoa mimea inayoonyesha dalili za kushambuliwa.
  • ·         Nyunyuzia majivu kwenye vikonyo ili kuua larva kwenye mimea iliyoshambuliwa
  • ·         Tumia kilimo mchanganyiko wa zao la mahindi na jamii ya mikunde
  • ·         Kilimo mzunguko kwa kubadilisha mazao jamii moja na nyingine
  • ·         Epuka kusafirisha mimea/mazao kutoka shamba lililoathirika na Kiwavijeshi Vamizi


  Udhibiti wa kutumia Viuatilifu
  • ·         Kagua shamba kubaini uwepo wa lava wa Kiwavijeshi Vamizi kwenye shamba
  • ·         Tumia viatilifu vilivyosajiliwa Tanzania kwa kufuata maelekezo kwenye kibandiko kilichopo kwenye kifungashio.
  • ·         Kiuatilifu kipulizwe wakati wa asubuhi au jioni kwenye eneo lililoshambuliwa na Kiwavijeshi Vamizi
  • ·         Kwa ushauri unaweza kutumia kiuatilifu chenye usajili wa jina la DUDUBA EC, Belt 480SC, Emamectin benzoate au Mupacron 50EC, DUDUALL, PROFECRON n.k
  • ·         Matumizi ya kiuatilifu iwe ni hatua ya mwisho baada ya mbinu nyingine kushindwa
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Post a Comment

  Item Reviewed: KIWAVI JESHI VAMIZI [Fall Armyworm] MDUDU HATARI KWA ZAO LA MAHINDI Rating: 5 Reviewed By: Kilimo mifugo
  Scroll to Top